Saturday, August 20, 2016

Usain Bolt amehitimisha career yake kwenye Olimpiki baada ya kuchukua medali ya tatu ya dhahabu ya mita 4x100 ambayo ilikuwa ni ya kupokezana vijiti kwenye mashindano ya mwaka huu na ya tisa tangu alipoanza kushiriki.

Bolt, 29, hapo awali ameshinda mbio za mita 100 na 200 na amekuwa mwanaridha pekee alyeshinda mbio zote tatu kwenye mashindano matatu.

Alikuwa pamoja na Asafa Powell, Yohan Blake na Nickel Ashmeade kumaliza sekunde 37.27.

Japan wameshinda medali ya ya shaba bila kutarajia huku USA wakiondolewa na ushindi wao wa medali ya fedha kupewa Canada na Uingereza kushika nafasi ya sita.

"Mpooo!!. Mimi ni bora," alisema Bolt, baada ya kumaliza mashindano hayo kwa kishindo.

Mwezi Februari, Bolt alithibitisha kuwa angestaafu mwaka 2017 baada ya Mashindano ya Dunia yatakayofanyika jijini London, na hatakuwepo kwenye mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika jijini Tokyo mwaka 2020, wakati ambapo atakuwa na miaka 34.

Bolt amejikusanyia medali tisa katika historia ya michuano hiyo, akifungana na wababe wengine wa USA Carl Lewis na Paavo Nurmi.

"Nitachelewa kuondoka ili nifurahi na washabiki wangu. Sikutarajia kama hili lingetokea wakati nilipokuwa naanza," alisema Bolt.

"Watu wengi walikuwa nyuma yangu wakinisapoti. Na kwa kuwa tumepata ushindi, basi ni jambo la kushukuru."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video