Baada ya tetesi za mshambuliaji wake tegemeza Sergio Aguero kufungiwa michezo mitatu endapo atakutwa na hatia ya kumpiga kiwiko kwa makusudi bei wa Wes Ham Winston Reid, meneja wa Man City Pep Guardiola amesema: ‘Sikuliona tukio lile, hivyo siwezi kusema chochote.’
‘Natumaini hakuna baya litakalotokea. Na kama litatokea tutakubaliana nalo na kuendana nalo. Kama tutampoteza basi ndiyo tumempoteza hivyo.’
Bosi wa West Ham Slaven Bilic pia hakuona tukio hilo na kudai kwamba uamuzi wa kumtoa Reid ulikuwa umezingatia zaidi sababu za kiufundi.
‘Sikumtoa kwasababu ya tukio lile. Nilifanya vile kwasababu nilitaka kufanya madabiliko tangu awali,’ Bilic alisema.
0 comments:
Post a Comment