Mkutano mkuu wa mwaka wa Wanachama wa klabu ya Yanga SC, unatarajia kufanyika kesho ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia majira ya saa tatu asubuhi, japokuwa mpaka sasa Agenda zitakazojadiliwa hazijiwekwa hadharani.
Kinachoendelea kwa watu wengi wakiwemo wanachama wa Yanga ni kuhisi tu mambo yatayokuwepo kwenye mkutano na moja ya hisia kubwa ni kuwa huenda baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji wakafukuzwa kutokana na kumpinga mwenyekiti Yusuf Manji.
Mmoja ya Mjumbe aliyepo kwenye wakati mgumu ni Salum Mkemi ambaye Agosti 4 mwaka huu alisikika katika kituo cha Redio cha EFM kupitia kipindi cha Sports Headquarter akisema mkutano huo ni
batili kwakuwa umekiuka katiba ya Yanga, akidai hata wao Wajumbe wa kamati ya
Utendaji hawajapewa barua juu ya hilo na hawajui hata ajenda zitakazojadiliwa.
"Kwa mujibu wa katiba yetu, mwenyekiti anapaswa
kushauriana na kamati ya utendaji kuitisha mkutano mkuu wa dharura lakini
katika hili hakuna mwanachama mwingine yoyote aliyeshirikishwa sasa huu
sio utaratibu hauwezi kuongoza taasisi kwa matakwa yako binafsi," alisema
Mkemi.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alijibu tuhuma hizo kwa kusema endapo mwanachama yoyote ana duku duku anapaswa kwenda kuzungumza
katika mkutano mkuu na kufuata utaratibu wa kuongea na viongozi sio kulalamika
kwenye vyombo vya habari.
"Hata hao wajumbe ni viongozi kama sisi, tulichaguliwa
siku moja na wanachama kwahiyo kama wanaona kuna mapungufu sehemu wanatakiwa
kufuata utaratibu na sio kulalamika ilibidi aje kwenye mkutano huo
azungumze," alieleza Sanga.
Wanachama wa Yanga wanaelekea kufanya mkutano siku chache tu baada ya watani zao Simba SC kufanya Mkutano mkuu wa Wanachama (Julai 31 mwaka huu) katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Osterbay, Dar es salaam ambapo agenda kubwa ilikuwa kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wanachama wa kawaida hadi kuingia kwenye mfumo wa Hisa na tayari Mwanachama mmoja na Mfanya biashara maarufu nchini, Mohamed Dewji 'Mo' ameshatangaza kuhitaji asilimia 51 za hisa kwa ofa ya Shilingi Bilioni 20.
Je, Yanga wao wataibuka na nini kesho?....ni jambo la kusubiri.
0 comments:
Post a Comment