Sunday, August 14, 2016

Klabu ya KRC Genk anayoicheza nahodha wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, jana usiku imeshindwa kutamba mbele ya Waasland Beveren baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 kwenye mchezo wa ligi ya Ubelgiji (Pro League).
Genk walitoka nyuma kwa magoli 2-0 hadi kusawazisha na kuambulia pointi moja katika mchezo huo. 
Nikolaos Karelis aliifungia Genk goli la kwanza dakika ya  35 kabla ya mchezaji wa Waasland Beveren Laurent Jans  kujifunga na hatimaye kuisawazishia Genk. 
Magoli ya Waasland Beveren yaliwekwa kambani na Ibrahima Seck aliyefunga dakika ya 6 na Jonathan Buatu ambaye alifunga bao la pili.
Katika mchezo huo Samatta aliingia dakika ya 47 kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kebano.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya tatu katika ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupilier Pro League) ambapo hadi sasa Genk inakamata nafasi ya 6 ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi tatu ikifanikiwa kushinda mechi moja, sare moja huku ikipoteza mchezo mmoja.
Hapa chini ni matokeo ya mechi zote za jana,  ratiba ya leo na Msimamo mpaka sasa:

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video