Friday, August 5, 2016

KRC Genk ya Mbwana Samatta imezidi kuchanja mbuga katika michezo ya mtoano kufuzu kucheza Michuano ya Europa baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 ugenini dhidi ya Cork City katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Turner's Cross, mjini Cork huko nchini Ireland usiku wa kuamkia leo.
Genk ambao leo walionekana kuwa kwenye kiwango bora na kuwapa shida wenyeji wa mchezo huo Cork City waliandika bao la kwanza dakika ya  13 kupitia kwa mlinzi wao Thomas Buffel na baadaye kuandika bao la pili kupitia kwa Sebastien Dewaest mnamo dakika ya 42.
Genk walienda mapumziko wakiwa na hazina ya mabao 2-0 dhidi ya wenyeji wao.
Kipindi cha pili Cork City walikuja kwa kasi ya aina kwa nia ya kusawazisha na pengine kuibuka na ushindi na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Alan Bennett 63. 
Cork walindelea na juhudi za kusaka bao lingine lakini hata hivyo juhudi zao hazikuzaa matunda.
Kwa matokeo hayo Genk wamefanikiwa kusonga mbele kwa wastani wa mabao 3-1, kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa awali uliopigwa maskani yao.
Genk sasa wanavuka kuelekea hatua ya mwisho ya mechi za mtoano, ambapo wakifuzu wataenda moja kwa moja sasa kwenye hatua ya makundi na kukutana na vigogo kama Manchester United, West Ham na wengineo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video