Kumekuwa na majibizano mazito kwenye Twitter kati ya Allan Shearer na Rio Ferdinand juu ya Wayne Rooney na uwepo wake kwenye timu ya taifa ya England.
Shearer, ambaye ni nahodha wa zamani wa England alistaafu kuchezea timu ya taifa akiwa na umri waka miaka 29, na kuwa mchezaji aliyestaafu mapema zaidi kuchezea taifa hilo tena akiwa kama nahodha.
Shearer anaamini kwamba Rooney anatakiwa kustaafu kutokana na umri kumtupa mkono na mwili wake kuchoka kutokana na kuitumikia timu hiyo tangu akiwa na umri mdogo kabisa.
Rooney alianza kuitumia England mapema kabisa akiwa na umri wa miaka 16, hivyo Shearer anaamini kwamba endapo Rooney ataamua kustaafu sasa hivi, atakuwa na wakati mzuri wa kuvuta nguvu na kufanya vyema kwenye klabu yake ya Manchester United.
Rio hakubaliani na Shearer
Mchezaji mwenza wa zamani katika klabu ya Manchester United Rio Ferdinand ametofautiana mtazamo na Shearer juu ya suala la Rooney kustaafu.
Kupitia kaunti yake ya Twitter Rio ameonekana kupingana na Shearer juu ya suala hilo.
Na haya ndio majibizano yao
0 comments:
Post a Comment