Tuesday, August 9, 2016

KOCHA wa Real Madrid Zinedine Zidane ameamua kuwatoa Toni Kroos na Gareth Bale kutoka kwenye Kikosi ambacho leo Agosti 9 kitakuwa huko Norway kucheza Mechi ya UEFA SUPER CUP dhidi ya Sevilla.
UEFA SUPER CUP ndio Mechi rasmi ya kufungua msimu wa Mashindano ya Klabu ya UEFA huko Ulaya na huchezwa  kati ya Bingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI, ambaye sasa ni Real, na aliyetwaa EUROPA LIGI ambaye ni Sevilla, zote zikiwa toka Spain.
Bale na Kroos sasa wanaungana na Cristiano Ronaldo na Pepe kuwa nje ya Kikosi cha Real kilichopo kambini hivi sasa kutokana na kupewa mapumziko ya ziada kutokana na maumivu yao.
Lakini upo uwezekano wa Straika Karim Benzema kucheza ikiwa Zidane ataamua baada ya Mfaransa huyo kutocheza hata Mechi moja kati ya 3 walizocheza Real hivi karibuni katika matayarisho yao.
Wengine ambao wanaweza kupewa namba kwenye Mechi hii na Seville licha ya kuchelewa kuingia kambini ni Luka Modric, James Rodriguez na Sergio Ramos.
Licha ya kuwakosa Mastaa hao wakubwa Wanne ambao ni wa Kikosi cha Kwanza Zidane ana Kikosi imara na huenda Golini akaanza Casiila, Mabeki kuwa Carvajal, Ramos, Varane na  Marcelo, Viungo kupiga Casemiro, Isco na Modric wakati Morata, Vázquez na James wakicheza Fowadi huku Benzema akianzia Benchi.
REAL - KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI:
MAKIPA: Casilla, Yáñez, Luca
MABEKI: Carvajal, Ramos, Varane, Nacho, Danilo, Marcelo
VIUNGO: James, Casemiro, Kovacic, Modric, Isco, Asensio, M. Llorente
MAFOWADI: Benzema, Lucas Vázquez, Morata, Mariano.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video