Mchana wa
leo zimeripotiwa Taarifa za Mshambuliaji Mkongwe wa klabu ya Simba, Musa Hassan
Mgosi kustaafu rasmi soka na kupewa nafasi ya Umeneja wa klabu hiyo.
MPENJA
SPORTS imemtafuta Mgosi na kumuuliza juu ya taarifa hizo na maelezo yake ni haya: “Kwanza
napenda kukanusha suala lililoandikwa kwenye mitandao la Mgosi kustaafu, Mgosi
kama Mgosi, suala la kustaafu mpira bado sana, Pogba (Paul) atakapostaafu ndipo
atafuatia Mgosi kustaafu”. Amesema Mgosi na kuongeza”
Hata hivyo,
Mgosi ameonesha wazi yuko tayari kufanya kazi yoyote ndani ya Simba hata kama
atakuwa nje ya uwanja, kitu kinachoashiria yuko mbioni kutundika daluga.
“Mimi ni mchezaji wa Simba, ni Mfanyakazi wa
Simba, nipo tayari kufanya majukumu yoyote yanayoihusu Simba, aidha katika
uchezaji au sekta nyingine”.
Mgosi
anayeheshimika ndani ya Simba amesema kutekeleza majukumu mengine nje ya
kucheza ndani ya Simba alishaanza msimu uliopita, lakini hakuna aliyehusisha na
kustaafu soka.
“Kuisaidia
Simba nje ya uwanja nimelifanya hilo toka mwaka jana, lakini mbona
halijaandikwa hivyo, mwaka jana nimekuwa msaidizi wa Mayanja (Jackson), nilimsaidia kila
kitu kama kocha msaidizi”. Amesisitiza Mgosi na kufafanua: “Unapozungumza mtu
kistaafu tuwe na subira, lazima niseme mwenyewe, sio mitandao iandike, wengine
wanaandika wapate comments, likes na kushtusha watu ambao wananihitaji.”
MPENJA SPORTS imemuuliza kama anaamini muda wa
kustaafu umefika na yuko tayari kuwa Meneja wa Simba.
“Sio tatizo, ni jukumu ambalo nitalifanyia kazi kwa vile
ninavyofahamu mimi, ukitaka kuangalia kiongozi anayeweza kuingoza Simba kwa
kila kitu, hakuna mtu ambaye kwa haraka unaweza kumuangalia zaidi ya Mgosi, kwasababu ni mtu ninayeheshimika na wachezaji,
naheshimika na mashabiki, naheshimika na viongozi wa Simba, naamini katika
sekta yoyote nitakayopewa Simba, hakuna atayepinga, kwahiyo najivunia klabu
yangu ya Simba.”. Ameongeza Mgosi.
Licha ya
kakanusha kustaafu rasmi, taarifa za ndani ambazo MPENJA SPORTS imezipata ni kuwa
kweli Mgosi anaelekea kustaafu na mechi ya Jumapili dhidi ya URA itakuwa maalum
kwake kuagwa, lakini yeye mwenyewe na uongozi hauko tayari kulizungumzia
kwasababu kuna masuala kadhaa wanajadiliana.
Inaelezwa
keshokutwa Jumamosi, Mgosi atakutana na
viongozi wa Simba kujadili suala la nafasi wanayotaka kumpa ikiwemo kuandaa
mkataba .
0 comments:
Post a Comment