Thursday, August 18, 2016

Umepita muda mrefu sasa tangu klabu ya Manchester United kukosa mtu sahihi wa kuongoza safu ya ulinzi, mtu mwenye roho ngumu, mtu asiyetaka kuona uchafu ukizaa langoni mwake (non-nonsense defender). Tangu kuondoka kwa Nemanja Vidic na Rio Ferdinand United wamekuwa wakiyumba kwenye safu yao ya ulinzi.

Sasa kuna sura mpya nyeusi imekuja, sura isiyo na masihara, sura yenye kila sifa ya kupewa dhamana ya kuongoza safu ya ulinzi. Huyu si mwingine bali ni Eric Bailly, Muivory Coast aliyesajiliwa akitokea klabu ya Villa Real ya nchini Uhispania.

Akiwa ameshacheza michezo miwili tu ya ushindani, Eric Bailly ameonesha ukomavu wake na kuwa shujaa kwa mashabiki. Ameonesha vitu vingi vinavyodhihirisha uwezo wake mkubwa wa kuimudu vyema safu ya ulinzi, utulivu, uwezo mkubwa wa kwenda na kasi ya mchezo na matumizi makubwa ya akili.

Ulikuwa ni usajili wa kwanza kabisa wa Jose Mourinho kwa paundi mil 30 na baadaye kufuatiwa na Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na sasa Paul Pogba.

Ilikuwa si rahisi kuamini uwezo wake kutokana na ukweli kwamba, hakuwa akitajwa sana kwenye dirisha la usajili. Lakini tayari ameonesha kwamba nini United walikuwa wakikosa kwa muda mrefu.

"Alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Leicester, lakini alisema hakuna shida na kucheza dakika zote 90. Halafu siku iliyofuata alishindwa kufanya mazoezi," Mourinho aliwaambia wanahabari baada ya ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Bournemouth. 

“Na alifanya mazoezi tena kwa mara ya kwanza Ijumaa. Wiki nzima hakufanya na wenzake kwasababu ya tatizo lake hilo.

“Tunajiona ni wenye bahati kwasababu amefanya kazi kubwa sana huku akiwa amefanya mazoezi kamili siku moja tu kabla ya mechi na kuonesha uwezo mkubwa.”

Ni mchezaji ambaye hahofii kupambana kweye mipira ya juu, uwezo wake wa kupiga tackles, kasi yake na ubora wa hali ya juu kwenye kumiliki mpira ukiwa kwenye himaya yake. 

Hii ndiyo kusema kwamba, Bailly ni beki aliyekamilika katika nyakati hizi ambazo hahitajiki tena beki mwenye 'kubutuabutua' ukizinagtia kwa sasa ana umri wa miaka 22 tu.

Kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester licha ya kupata kadi ya njano, lakini haikumfanya kupunguza kasi yake ya kukaba uwanjani. Na alicheza muda wote akiwa na utulivu hadi mwisho wa mchezo.

Kiungo wa zamani wa Liverpool Jamie Redknapp hakusita kumimina pongezi kwa beki huyo na kusema kwamba, uchezaji wake kwa kiasi kikubwa unaweza hata kusaidia kuimarisha eneo la safu ya kiungo ya Man United.

"Ni mchezaji anayeweza kucheza hata eneo la kiungo. Mara kadhaa nimemwona akichukua mpira na kusogea nao mpaka kwenye eneo la kiungo, ana kasi, kimsingi hana mapungufu yaliyo dhahiri. Kwa hakika washabiki wa Manchester United watampenda sana." alisema Redknapp

"Ni beki mzuri sana. Hafanyi makosa ya wazi, kama akiamua kwenda kwa adui anafanya kweli na wala hasiti kuchukua maamuzi. Yuko imara sana, na kwa hakika United hawajapoteza pesa zo kumnunua beki huyu."

"Kabla ya mchezo, nilidhani wangepata matatizo mengi sana kutokana na wepesi wa safu ya ushambuliaji ya Bournemouth, lakini haikuwa kama nilivyodhani. Kulikuwa na utulivu wa hali ya juu na hasa kwa upande wa Bailly."

Tangu kuondoka kwa kamanda Nemanja Vidic, United walikuwa wakihangaika sana kutafuta watu sahihi wa kuziba nafasi hiyo, walitengeneza partnership ya Phil Jones and Jonny Evans lakini ilishindwa. 

Wakaja na Tyler Blackett na Paddy McNair mambo yakawa bado, Marcos Rojo na Daley Blind hali haikuwa shwari kabla ya Smalling kuonesha dalili za kumudu nafasi hiyo vyema na sasa ujio wa Bailly wakishirikiana na Smalling basi tunaiona United nyingine msimu huu, United ambayo safu yake ya ulinzi haitakuwa na mushkir.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video