Ligi kuu ya soka ya England imerejea rasmi na mabingwa watetezi Leicester City wamefungua dimba kwa kuchapwa 2-1 na wenyeji Hull City.

Hull City walianza kuliona lango la Leicester dakika ya 45' kupitia kwa Adama Diomande, lakini Riyad Mahrez akasawazisha dakika ya 47.

Bao la ushindi kwa Hull limetiwa kambani dakika ya 57 na Robert Snodgrass.
Hull City wameonja kukaa kileleni kwa muda wakati wanasubiri mechi nyingine zinazopigwa sasa:

Mahrez ameanza ligi kwa kufunga goli
0 comments:
Post a Comment