Ligi nne kuu za mataifa ya bara Ulaya zinazoongoza zitatengewa nafasi nne kila moja katika hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuanzia msimu wa 2018-19.
Ligi hizo ni za England, Ujerumani, Italia na Uhispania.
Chini ya mfumo wa sasa, England, Ujerumani na Uhispania huwa na nafasi tatu, huku klabu zinazomaliza nambari nne ligini zikilazimika kucheza hatua ya muondoano wa kabla ya makundi.
Italia imekuwa na nafasi mbili pekee za uhakika, na nyingine moja ya kufuzu kabla ya hatua ya makundi.
Mshindi wa ligi dogo ya Ulaya, Europa League, pia atahakikishiwa nafasi hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashindano wa Uefa Giorgio Marchetti, mpangilio wa Ligi ya Mabingwa hata hivyo utabaki vilevile.
Baada ya hatua ya kufuzu, klabu 32 zitapangwa katika makundi manane ya klabu nne ambazo zitapigania nafasi ya kuingia hatua ya muondoano ya klabu 16.
0 comments:
Post a Comment