
Utamu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya sasa uko njiani kurejea ambapo droo ya upangaji makundi usiku wa leo jijini Monaco ambako ndipo makao makuu ya Uefa yalipo.
Mbali na droo hiyo, pia kutakuwa na zoezi lingine la kutangaza Mchezaji Bora Ulaya msimu wa
2015/16, ambapo kwenye kinyang'anyiro hiko wamo wachezaji watatu tu ambao ni Cristiano Ronaldo na Gareth Bale (Real Madrid), na Antoinne Griezmann (Atletico Madrid).
Majira saa ya moja za usiku kwa saa za Afrika Mashaiki ndiyo muda ambapo droo hiyo itafanyika, ambapo kuna jumla ya timu 32 ambazo zimepangwa kwenye vyungu vinne vyenye timu 8 kila kimoja ili kupanga Makundi 8 ya Timu 4 kila moja.
Chungu namba 1 kina Mabingwa Watetezi Real Madrid na Mabingwa wa nchi 7 ambazo ndizo zinazopewa kipaumbele kwenye listi ya upangaji makundi ya ligi hiyo.
Kwa kuanzia na kanunu chache za droo hiyo
- Timu kutoka nchi moja hazitapangwa kundi moja.
- Timu kutoka Russia na Ukraine hazitapangwa kwenye kundi moja.
Namna timu zilivyogawanywa kwenye vyungu vinne.
Chungu cha kwanza
Real Madrid, Barcelona, Leicester City, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Paris Saint-German, CSKA Moscow
Chungu cha pili
Atletico Madrid, Borussia Dortmund, Arsenal, Manchester City, Sevilla, Porto, Napoli, Bayer Leverkusen
Chungu cha tatu
Tottenham, Dynamo Kiev, Lyon, PSV Eindhoven, Sporting Lisbon, Club Bruges, Basle, Monchengladbach
Chungu cha nne
Monaco, Besiktas, Legia Warsaw, Ludogrets, Celtic, Rostov, Cophenagen, Dinamo Zagreb
Tarehe ambazo mechi za makundi zitachezwa
Mechi ya 1: 13–14 Septemba
Mechi ya 2: 27–28 Septemba
Mechi ya 3: 18–19 Oktoba
Mechi ya 4: 1–2 Novemba
Mechi ya 5: 22–23 Novemba
Mechi ya 6: 6–7 Desemba
0 comments:
Post a Comment