Leroy Sane amekamilisha usajili wa kujiunga na Manchester City kwa dau la paundi milioni 37 akitokea klabu ya Schalke ya Ujerumani.
Nyota huyo mwenye miaka 20 amesaini mkataba wa miaka mitano na amekabidhiwa jezi namba 19.
Sane ambaye ni usajili wa sita msimu huu kwa wakali hao wa Etihad chini ya kocha Pep Guardiola amethibitisha kwamba fursa ya kufanya kazi na bosi huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich ndio sababu ya maamuzi yake ya kumfuata kutoka Bundesliga kwenda ligi kuu ya England.
"Moja ya sababu iliyonifanya niamue kujiunga na City (Manchester) ilikuwa Pep Guardiola,'Amesema Sane. "Alinishawishi kuja hapa kwa kuwa naweza kuendelea mbele. Najua nitajifunza mengi chini yake na sasa naweza kupiga hatua nyingine katika maisha yangu ya soka".
0 comments:
Post a Comment