Saturday, August 13, 2016

Mchezo wa nane bora kati ya Yanga dhidi ya MO Bejaia unatarajia kupigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, wakati Yanga inaingia uwanjani kutupa karata yake ya tano ikiwa na pointi moja, ikumbukwe Yanga ilifungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa awali uliopigwa Algeria.

Mlinda mlango wa Yanga Deogratius Minishi ‘Dida’ ameuzungumzia mchezo dhidi ya MO Bejaia: “Tunawaomba mashabiki wetu wasikate tamaa, tupo pamoja nao hii ndiyo timu yao na wanatakiwa kuja kuipa sapoti mwanzo mpaka mwisho. Wanatakiwa wajivunie timu yao kufika katika hatua hii, ni jambo la heshima waendelee kuiamini timu yao na kuiunga mkono Mungu akitujaalia kwenye mechi dhidi ya MO Bejaia tunaweza kupata ushindi.”

Alipoulizwa kama wametawaliwa na uchovu kwasababu hawajazoea kucheza kwa muda mrefu na imekuwa kawaida ligi ikimalizika wanapumzika, Dida amejibu:

“Hilo kweli lipo lakini tutajitahidi tuweze kupata hata ushindi kwenye mechi moja lakini naamini madaktari wetu na waalimu wanazidi kutupa nafasi ya kupumzika na kutupa huduma za hapa na pale ili tuwe vizuri siku hadi siku. Mimi naamini tangu tumeingia kwenye mashindano haya, tumekutana na changamoto kadhaa kama kusafiri mara kwa mara, mazoezi mfululizo na mechi mfululizo, lakini ni fundisho kwetu kwenye msimu ujao.”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video