Manchester City wamefanikiwa kukamilisha usajili wa kinda Mkolombia Marlos Moreno, klabu imetangaza leo.
Moreno (19) amesaini mkataba wa miaka mitano akitokea klabu ya Atletico Nacional
Hata hivyo mshambulizi huyo anakwenda moja kwa moja kwa mkopo kunako klabu ya Deportivo La Coruna ya Uhispania kwaajili ya msimu wa 2016-17.
"City ni moja ya vilabu bora ulimwenguni kwa sasa," aliiambia tovuti ya klabu.
0 comments:
Post a Comment