Silva alikuwa sehemu ya kikosi cha Ureno kilichoshinda taji la Kombe la Mataifa ya Ulaya |
Kiungo wa Sporting Lisbon na Ureno, Adrien Silva, amethibitiha kuwa atajiunga na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka ya England, Leicester City.
Nyota huyo aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Ureno kilichotwaa ubingwa wa Uefa Euro 2016 nchini Ufaransa, amedai ataondoka Sporting kwenda ligi kuu ya England kwa ada inayoripotiwa kuwa paundi milioni 21.
Silva ana mpango wa kuungana na mchezaji mwenzake wa Sporting, Islam Slimani aliyetimkia The King Power Stadium , lakini mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka Leicester City juu ya taarifa hizo za Silva.
0 comments:
Post a Comment