Saturday, August 6, 2016

Sunderland imemsajili Papy Djilobodji  kwa paundi milioni 8 akitokea klabu ya Chelsea.
Mlinzi huyo ambaye majira ya kiangazi mwaka jana aliwasili Stamford Bridge kutokea klabu ya  Nantes amesaini mkataba wa miaka minne na anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Sunderland, David Moyes.
Nusu ya pili ya msimu uliopita, Djilobodji alicheza kwa mkopo katika timu ya Werder Bremen na kuisaidia timu hiyo kubaki salama katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga.
Mchezaji huyo, 27, aliichezea mechi moja tu Chelsea, lakini bado ameuzwa kwa £8million
Chelsea wamepata faida ya karibia paundi milioni 6 kutoka kwenye mauzo ya beki huyo wa kati ambaye walimnunua kwa dau la paundi milioni 2.2.

Mechi hiyo moja aliyoichezea Chelsea tena akiingia dakika za mwisho akitokea benchi ilikuwa ya Capital One iliyochezwa mwezi Septemba mwaka jana .

Djilobodji, Raia wa Senegal ameichezea timu yake ya Taifa mechi 13 na alikuwepo katika michuano ya mataifa ya Afrika mwaka jana.   
Baada ya kusajiliwa, Djilobodji aliiambia Tovuti ya klabu ya Sunderland: "Nina furaha sana kujiunga na Sunderland, naamini tunakwenda kufanya kitu fulani mwaka huu".

HAPA CHINI NI TAKWIMU CHACHE ZA MCHEZAJI HUYO:

06 Aug 2016

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video