Tuesday, August 16, 2016

Diego Costa slotted Chelsea's winner one minute from time to get Antonio Conte's off to a flyer
Diego Costa akishangilia baada ya kufunga goli la ushindi

Goli la jioni la Diego Costa limempa kocha wa Chelsea Antonio Conte ushindi wake wa kwanza katika mechi ya ufunguzi wa Ligi ya England baada ya kuichapa West Ham magoli 2-1.

Costa alifunga goli hilo dakika ya 89 kufuatia shuti kali alilopiga kutoka mita 20 na kumpa wazimu Conte ambaye alienda kushangilia na washabiki wake katika dimba la Stamford Bridge

Eden Hazard ndiyo alifunga goli la kwanza la Chelsea dakika ya 47 kwa njia ya penati baada ya beki wa West Ham Michail Antonio kumchezea madhambi Cesar Azpilicueta.

Beki wa West Ham James Collins akasawazisha goli dakika ya 77 baada ya kumalizia mpira uliokuwa ukizagaa langoni mwa Chelsea kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Dimitri Payet.

Kante and Hazard wang'ara

Matumaini ya Chelsea kuonesha dalili za kuwa katika mbio za ubingwa msimu huu bado liko hai kutokana mchezo mzuri waliouonesha dhidi ya mahasimu wao wa jadi. Walimiliki mpira kwa asilimia 62 huku West Ham wakimiliki asilimia 38.

Lakini ukiachana na hilo, kazi iliyofanywa na kiungo wa Mfaransa aliyenunuliwa kwa paundi mil 30 N'Golo Kante, ambaye msimu uliopita alichukua ubingwa akiwa na Leicester na kurudi kwa Hazard kwenye kiwango chake ilikuwa ni chachu kubwa ya ushindi wa Chelsea.

Hazard alionekana kuwa na kasi na mwepesi huku akifanya ubunifu wa hali ya juu na kuipa shida safu ya ulinzi ya West Ham, licha ya baadaye kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Victor Moses.


Mshambuliaji Michy Batshuayi pia alionesha viashirio chanya kutokana na kuonesha kiwango kikubwa licha ya kuingia dakika za mwisho kabla ya mchezo kumalizika. Yeye ndiye aliyetoa pasi ya kichwa na kumfikia Costa ambaye alifunga bao la ushindi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video