Zikisalia saa chache kabla ya Dirisha la Usajili la majira ya joto kufungwa usiku wa leo, Chelsea wamefanya 'Sapraiz' baada ya kuripotiwa wakitaka kumrudisha Stamford Bridge, beki wao wa zamani David Luiz kwa ada ya pauni milioni 32.
David Luiz akiwa na Chelsea alishinda kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi ya Europa |
Mbrazil huyo aliondoka Chelsea Juni 2014 na kujiunga na Paris Saint-Germain kwa dau lililovunja rekodi ya Dunia kwa usajili wa mabeki ambalo lilikuwa pauni milioni 50, lakini sasa yuko tayari kurejea Magharibi mwa London.
Chelsea inahaha kutafuta beki wa kati hasa baada ya kukataliwa kuwasajili Alessio Romagnoli wa AC Milan na mlinzi wa Napoli, Kalidou Koulibaly.
0 comments:
Post a Comment