Sportsmail wameripoti, Chelsea wako tayari kutoa ofa ya mchezaji Loic Remy jumlisha na mkwanja wa paundi milioni 65 ili kuinasa saini ya Romelu Lukaku.

Taarifa zinadai kuwa Everton wamekubali straika huyo wa Ubelgiji, 23, aondoke Goodison Park, lakini wamekomalia paundi milioni 75 lazima zitoke ili kuvunja mkataba wake ambao amebakia miaka mitatu.
Mwezi Januari mwaka huu, Remy alikuwa kwenye rada za Mkurugenzi wa Everton, Steve Walsh, labda inaweza kuwasaidia pia Chelsea.

Hata hivyo Everton imesema bado haijapokea ofa rasmi kutoka Chelsea, pengine kikwazo ni kiasi kikubwa cha pesa wanachohitaji..
Chelsea wanataka kumrudisha Lukaku waliyemuuza mwaka 2014 kwa dau la paundi milioni 28.
0 comments:
Post a Comment