Kocha mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm leo anatarajiwa kumchezesha winga mwenye kasi, Juma Mahadhi 'Neymar'.
Nyota huyo aliyesajiliwa majira haya ya kiangazi akitokea Coastal Union ya Tanga, kwenye mazoezi ya mwisho ya Yanga yaliyofanyika juzi uwanja wa Taifa alionesha vitu vya aina yake.
Mashabiki wa Yanga wanafananisha uwezo wa Mahadhi na mshambuliaji hatari wa Barcelona na Brazil, Neymar da Silva Santos Junior.
Umekuwa utamaduni wa kawaida kwa wachezaji wa Kibongo kubebeshwa au kujibebesha majina ya wachezaji wakubwa wa Ulaya.
Nadir Haroub anaitwa Cannavaro, beki wa zamani wa Italia, Haruna Niyonzima anaitwa Fabregas, kiungo mahiri wa Hispania na Chelsea, Kelvin Yondani anaitwa Vidic, kitasa cha zamani cha Manchester United na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment