Neymar na Gabriel Jesus wame-post picha Instagram
Neymar na mchezaji mwenzake wa Timu ya Taifa ya soka ya Brazil, Gabriel Jesus wameonesha tattoo zao zinazofanana wakati huu wawili hao wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki ya Rio 2016.
Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar ameonesha tattoo yake aliyochora mkono wa kushoto ikimuonesha nyota kinda akitazama mji fulani ambao huenda ni ule aliozaliwa wa Mogi das Cruze ambako alikuwa na ndoto ya kucheza soka, kujenga nyumba mpya na kushinda kombe la ligi ya mabingwa Ulaya.
Hata hivyo imeonekana straika wa Palmeiras ya Mexico, Jesus amekopi tattoo ya Neymar ikiaminika kuwa na maana ile ile.

0 comments:
Post a Comment