Friday, August 12, 2016

Lionel Messi amethibitisha nia yake ya kurejea timu ya taifa kwa mujibu wa kauli ya aliyoitoa leo.

Nyota huyo wa Barcelona alifanya uamizi wa kustaafu soka la kimataifa baada ya kupoteza mchezo wao wa fainali ya Copa America dhidi ya Chile mwaka 2016.

Baada ya kufanya mazungumzo na kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza, Messi amfikia uamuzi wa kurejea tena kwenye timu ya taifa.

"Naona kuna matatizo mengi kwenye soka la Argentina na nisingependa kuona yanaongezeka," amesema. leo

"Sitaki kuleta maafa, siku zote nimekuwa nikijitahidi kufanya kila niwezalo kuisaidia timu.

"Tunapaswa kutatua mambo mengi sana katika soka la Argentina, lakini natakiwa kufanya hilo nikiwa ndani ya timu na sio kukosoa nikiwa nje."

"Wakati wa fainali ile, nilikuwa na msongo wa mambo mengi sana kichwani mwangu na kikukweli niliamua kuachana na timu ya taifa, lakini mapenzi yangu kwa nchi hii na hii jezi yamenifanya nirudi," amesema. 

"Nadhani watu wote ambao wanataka mimi kuendelea kuwaepo kwenye timu ya taifa, natumaini sasa tutafurahia pamoja."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video