Wednesday, August 3, 2016

Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Dar Young Africans leo kimeendelea na mazoezi kujiwinda na mechi ijayo ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya MO Bejaia ya Algeria itakayochezwa Julai 13 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Kocha msaidizi wa Yanga SC, Juma Mwambusi ameiambia MPENJA SPORTS kuwa timu nzima imechukia kufungwa  na haitaki kupoteza mechi nyingine ya nyumbani.

"Maandalizi yanakwenda vizuri kiukweli, kwasababu ni mechi ya nyumbani tena, kupoteza kwa kweli kila mtu kachukia, kwasababu haiwezekani tukapoteza mechi nyingine nyumbani kama tulivyopoteza mwanzo. Sisi hatujakata tamaa, kikubwa ni kuendelea na mapambano mpaka mwisho". Ameeleza Mwambusi akizungumza na MPENJA SPORTS.
Yanga ambao wamepoteza mechi tatu na kuambulia sare moja katika mechi nne za kundi A za kombe la Shirikisho  walizocheza mpaka sasa wataingia uwanjani wakiwa na uchungu wa kupoteza mchezo uliopita kwa kuchapwa mabao 3-1 na Medeama.
Pia wanaumia zaidi kwa kipigo cha 1-0 walichopata nchini Algeria dhidi ya wapinzani wao wajao, MO Bejaia na kile cha 1-0 dhidi ya TP Mazembe uwanja wa Taifa.
Pointi moja waliyonayo Yanga walipata kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Medeama kabla ya kwenda kufungwa nchini Ghana.
Katika hatua nyingine, Yanga kuhakikisha wanafanya vyema mechi ijayo, Jumamosi ya Juma hili watashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar uwanja wa Taifa, Dar Es salaam.

Picha kwa hisani ya Naipenda YANGA

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video