Mshambuliaji mpya wa Chelsea aliyesajiliwa kutoka Marseille Michy Batshuayi, amefunga magoli mawili na katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bristol Rovers na kutinga raundi ya tatu ya Kombe la EFL.
Goli lingine la Chelsea lilifungwa na Victor Moses.
Bristol Rovers walipata magoli yao kupitia kwa Peter Hartley dakika ya 34 na Ellis Harrison dakika ya 49
Huu ni mchezo wa tatu mfululizo wa kimashindano, ambao kocha wa Chelsea Antonio Conte ameweza kuendeleza rekodi yake ya ushindi.
Chelsea walimiliki mpira kwa kiasi kikubwa sana kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizi makubwa lakini kazi nzuri ya mlinda lango wa Bristol Rovers Steve Mildenhall iliwanyima wababe hao wa darajani ushindi mnono zaidi.
0 comments:
Post a Comment