Barcelona wamekamilisha usajili wa Paco Alcacer kutoka kwa mahasimu wao wa La Liga Valencia kwa mkataba unaotajwa kugharimu paundi mil 27, huku kukiwa na kipengele cha Barcelona kuongeza euro milioni mbili za ziada.
Alcacer (23) anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na msimu huu baada ya kufuzu vipimo vya afya jana Jumatatu na kusaini mkataba wa miaka mitano.
Valencia wameziba pengo la Alcacer kwa kumchukua kwa mkopo kinda wa Barcelona Munir El Haddadi.
Alcacer amekuwa mchezaji wa nne kwa miaka ya hivi kiaribuni kutoka Valencia na kujiunga na Barcelona akiungana na mlinzi Jordi Alba (2012) na Jeremy Mathieu (2014) pamoja na Andre Gomes ambaye amejiunga na Barca kwenye majira haya ya usajili.
Amefunga magoli 13 na kutoa assists sita akiichezea Valencia msimu uliopita huku akiwa mfungaji bora wa timu ya taifa ya Hispania katika mbio za kwania kufuzu kucheza fainali za Euro 2016 baada ya kufunga magoli matano.
Alitemwa kwenye kikosi cha mwisho kilichosafiri kwenda Ufaransa kwenye mashindano ya Euro 2016.
Alcacer hakujumuishwa kwenye kikosi cha Valencia kilichocheza dhidi ya Eibar Jumamosi iliyopita. Baada ya kichapo cha goli 1-0, kocha wa Valencia Pako Ayesteran aliwambia waandishi wa habari mchezaji huyo hakuwa kwenye wakati mzuri wa kushindana.
Usajili wa Alcacer umeangukia siku ambayo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa (August 30) ambapo ametimiza miaka 23.
0 comments:
Post a Comment