Huenda sasa amekubali!, Mario Balotelli ameagana na masela wake baada ya jana usiku kufanya mtoko maalumu Mjini Manchester.
Inaonekana wazi, Mshambuliaji huyo mtukutu alikuwa akiwaaga rafiki zake kuwa hawezi kuendelea kubakia Liverpool kwasababu Kocha Jurgen Klopp ameonesha wazi hamhitaji.
Ikisalia siku moja na saa kadhaa dirisha la usajili kufungwa Barani Ulaya, Inaelezwa kwamba Balotelli anakwenda kujiunga na Nice ya Ufaransa.
Balotelli alionekana ni mwenye furaha akiwaaga mashikaji zake ambao baada ya kupata msosi kwenye mgahawa wa Kiitaliano, walianza kupiga picha pamoja, kama sehemu ya kuangana.
0 comments:
Post a Comment