Friday, August 12, 2016


ORODHA  kamili ya nyota watakao kuwa sehemu ya kikosi cha City msimu ujao tayari imetoka  ikiwa na jumla ya wachezaji  28, wanne kati yao wakiwa wamepandishwa kutoka timu ya vijana,huku 7 wakiwa wamejiunga katika kipindi hiki cha usajili  wakitokea kwenye vilabu vingine.
Kwa mujibu wa meneja  usajili wa kikosi hiki, Frank Mfundo, nyota wengine watatu  kutoka mataifa ya nje  watatangazwa mara baada ya taratibu zao za uhamisho  kutoka vilabu walivyokuwa wanacheza huko kwenye mataifa yao kukamili.
“Hii ni orodha ya wachezaji ambao tayari taratibu zao zimekamilika na ni uhakika kuwa  watakuwa sehemu ya kikosi chetu msimu ujao, hapa majina ya wachezaji ambao tunatarajia kuwasajili kutoka nje ya nchi hatujayajumuisha kwa sababu taratibu zao bado hazijawa sawa, kwa kuwa muda bado upo tunaendelea kulifanyia kazi hilo na imani yetu kubwa  tutakamilisha yale machache yaliyobaki ili waweze kujumuika kikosini” alisema.
IMG-20160718-WA0044
Rajab Zahir
Akiendelea zaidi Bwana Mfundo, aliwataja  wachezaji hao ambao bado wanasubiri kukamilishwa kwa taratibu zao ili waweze  kujumuishwa kikosini kuwa ni Hemedy Murutabose aliyekuwa akaichezea Bujumbura City ya Burundi, Sankhani Mkandawile na Owen Chaima  waliokuwa wakicheza kwenye kikosi cha Big Bullet ya Malawi.
“Tuko kwenye hatua nzuri naamini kabla ya muda wa mwisho wa dirisha la usajili kufungwa hapo Sep 6 tutakuwa tushakamilisha kila kitu kuhusu wachezaji hao ambao  walikuwa wamependekezwa na kocha wetu Kinnah Phiri”, alimaliza.
IMG-20160718-WA0044

Wachezaji 7 wapya walio kwenye kikosi hiki cha City ni pamoja na Fikirini Bakari,na Ayoub Semtawa kutoka Coastal Union, Rajabu Isihaka na Omary Ramadhan ‘Barbatov’ waliotokea African Sports zote za Tanga, Rajabu Zahir aliyetokea Young African, Mohamed Mkopi kutoka Tanzania Prison  na Mark Frank Makolo aliyetokea Azam Fc.
Kwa upande wa wachezaji  waliopandishwa  kutoka timu ya  vijana wapo  Kenneth Kunambi, Michael Kerenge,Joshua Ibrahim, na Peter Mwangosi.
Orodha kamili ni kama ifuatavyo
Juma Kaseja Juma, Fikirini  Bakari, Hamis Msabila,John Jerome, John Kabanda,Haruna Shamte,Hassan Mwasapile,Mark Franco Makolo,Tumba Lui Sued, Peter Michael Mwangosi,Rajabu Zahiri Mohamed,Kenny Ally Mwambungu,Medson Absolom Mwakatundu,Hamidu Mohamed, na Ramadhan Seleman Chombo.
Wengine ni Rafael Daud,Ayoub Semtawa,Joseph Mahundi,Ditram Nchimbi,Joshua Ibrahimu ,Omary Ramadhan,Issah Nelson,Michael Kerenge,Mohamed Mkopi,Salvatory Nkulula,Rajabu  Abdallah, Geofrey Mlawa na Kenneth Kunambi.
City  imepangwa kuanza ugenini mchezo wake wa  kwanza wa ligi kuu ya Vodacom  ambapo itacheza dhidi ya ‘Wana Nkulukumbi’ Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ikiwa ni baada ya uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba mkoani Kagera kuwa bado kwenye matengenezo.
IMG-20160809-WA0032IMG-20160809-WA0032
Geoffrey Mlawa (mwenye mpira) na Tumba Sued, mazoezini jana,kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Nyassa, Matema Beach, Kyela.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video