Aliyekuwa Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche ame-post picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa kwenye muonekana wa jezi namba 10 ya klabu yake mpya , Al Nahdha ya Oman.
Tchetche aliyekuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Azam FC, tayari ameshawaaga mashabiki wa Lambalamba kama ambavyo MPENJA SPORTS iliweka habari hiyo mapema leo.
Uongozi wa Azam FC kupitia kwa Afisa habari wake, Jaffar Idd Maganga umethibitisha mchana huu kuwa sasa suala la Kipre limemalizwa vizuri baada ya viongozi wa timu zote mbili kukutana na kumalizana kwa kufuata kanuni za usajili.
Kwa maana hiyo, Azam FC imebariki kuondoka kwa Tchetche ambaye alionesha nia ya kuachana na matajiri hao wa soka la Bongo.
0 comments:
Post a Comment