Monday, August 8, 2016

Shkodran Mustafi
Kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka ya England, Arsenal wapo kwenye wakati mgumu katika safu yao ya Ulinzi baada ya kuumia kwa Gabriel na hali hiyo imeanza kumtisha zaidi kocha Arsene Wenger  wakati huu anajiandaa kufungua dimba la EPL dhidi ya  Majogoo wa Jiji Liverpool, Jumapili ya Juma hili.
Gabriel aliumia katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kati ya Arsenal na Manchester City na kushuhudia Washika Bunduki hao wa London wakiibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Hata hivyo taarifa zinasema kuumia kwa Mbrazil huyo kumeongeza juhudi kwa Wenger kuisaka saini ya mlinzi wa Valencia  Shkodran Mustafi kwa dau la paundi milioni 40.
Mjerumani huyo ni Mlinzi chaguo namba moja la Wenger katika mipango yake ya usajili majira haya ya kiangazi na alipoulizwa kama atamsajili, amejibu: "Nimeshalisema mara nyingi sana, tuko sokoni. Kiukweli sio soko rahisi kwetu, tuamini habari njema zitakuja".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video