Wednesday, August 17, 2016

AZAM FC wameibuka washindi na kutwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza kufuatia kuifunga Yanga kwa changamoto za mikwaju ya penati 4-1, baada ya kumaliza dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ndani ya dakika tisini, Yanga walianza kupata mabao yao kupitia kwa Mzimbabwe Donald Ngoma kwa njia ya penati na Amissi Tambwe, huku Azam wakisawazisha kupitia kwa beki wa kulia Shomari Kapombe na John Bocco kwa njia ya penati.
Ulipowadia wakati wa mikwaju ya penati, Azam walipata penati zao zote zilizopigwa na John Bocco, Himid Mao, Shomari Kapombe na Kipre Balou, huku Yanga wakipata moja iliyopigwa na kipa Deogratius Munishi wakati Haruna Niyonzima na Hassan Kessy wakikosa.
Yanga; Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi/Malimi Busungu dk81, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Simon Msuva dk67 dk na Donald Ngoma.
Azam; Aishi Manula, Isamil Adam, Bruce Kangwa, David Mwantika, Himid Mao, Jean Baptiste Mugiraneza, Shomary Kapombe, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Kipre Balou dk90, John Bocco, Shaaban Chilunda/Mudathir Yahya dk46 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Francesco Zekumbariwa dk46. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video