Wednesday, August 3, 2016

Matajiri wa soka la Bongo Azama FC, leo wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wanajeshi wa JKT Ruvu, katika mchezo uliochezwa kunako dimba la Azam Complex lililopo Chamazi nje  kidogo ya jiji la Dar es Salaam
Azama walianza kuliona lango la JKT Ruvu dakika ya 44 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Aggrey Moris kufuatia mchezaji wa Azam kufanyiwa mdhambi kwenye eneo la hatari.
Lakini bao la Hassan Materema wa JKT Ruvu katika dakika ya 64 lilizima ndoto za Azam kuendelea na wimbi lake la ushindi katika mechi za kirafiki za maandalizi ya msimu mpya.
Katika pambano hilo lililokuwa la kuvutia, timu zote mbili zilicheza kwa kiwango bora huku safu za ulinzi za pande zote mbili zikionekana kucheza kwa umakini mkubwa. 
Azam walionekana kuuchukulia mchezo huu wa majaribio kwelikweli, baada ya kufanya mabadiliko mengi ya wachezaji, huku wachezaji wengi wakichezeshwa katika nafasi tofauti na ilivyozoeleka.
Beki wa pembeni wa Azam aliyepona maradhi yake ya mapafu yaliyomweka nje takriban miezi mitatu, Shomari Kapombe leo pia alipata wasaa wa kucheza mchezo wa leo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video