Saturday, August 20, 2016

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, leo Jumamosi inatarajia kuanza rasmi patashika ya kuwania taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu 2016/17 kwa kuwakaribisha mahasimu wao African Lyon ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo utaanza saa 1.00 usiku, ambapo Azam FC itaingia dimbani ikiwa na morali kubwa baada ya kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii Jumatano iliyopita ikiifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90.

Mabingwa hao wataanza kibarua hicho wakiwa na benchi jipya la ufundi chini ya makocha kutoka moja ya nchi iliyoendelea kisoka duniani Hispania, wanaoongozwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya Santa Ursula ya Hispania pamoja na wasaidizi wake, wamekuja na soka jipya kabisa ndani ya Azam FC, ambalo ni la kushambulia kwa kasi kwa kupigiana pasi za haraka pamoja na kukaba kwa nguvu kwa pamoja pale timu inapopoteza mpira.

Wakiwa na wiki saba tu tokea waanze kuifundisha Azam FC, kimuonekano timu hiyo imeanza kuonyesha ufiti wa kucheza dakika zote kutokana na aina ya mazoezi waliyokuwa wakipewa katika maandalizi ya msimu huu huku pia ikianza kuzoea kucheza soka la kasi na kuwa na nidhamu ya mchezo.

Yeray azungumzia mchezo

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuhusu mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Yeray Romero, alisema ni jambo muhimu sana kushinda mechi hiyo ya kwanza huku akitanabaisha ya kuwa anakiamini kikosi chake kitaibuka na ushindi leo.

“Mechi ya leo itakuwa muhimu sana kwa sababu ni mwanzo wa ligi, namshukuru Mungu mechi iliyopita tumeshinda dhidi ya Yanga hiyo itawaongezea ari wachezaji ya kucheza vema mechi hiyo, uwezekano wa kushinda sisi upo cha msingi ni wachezaji wanapaswa kutulia uwanjani na kuweza kukifanya kile tulichokuwa tukiwafundisha, ni mategemeo yangu tutashinda,” alisema.

Alisema kuelekea mchezo huo wameifanyia marekebisho safu yao ya ushambuliaji kwa kuwapa mazoezi binafasi baada ya kuwa inapoteza nafasi nyingi za kufunga, huku akiamini ya kuwa uwezekano wa kufunga mabao utakuwepo leo.

Azam FC inaingia kwenye ligi ikiwa imesajili wachezaji wapya wanne wa kimataifa, ambao ni mabeki Daniel Amoah (Ghana), kiraka Bruce Kangwa (Zimbabwe) na winga Enock Atta Agyei (Ghana) atayeanza kuichezea Azam FC Januari mwakani pamoja na mshambuliaji Gonazo Bi Thomas (Ivory Coast).

Rekodi zao (Head To Head)

Hadi zinaingia kwenye mchezo huo msimu huu, Azam FC ikitoka kushika nafasi ya pili msimu uliopita na African Lyon ikirejea tena Ligi Kuu ikitokea Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu hizo zimekutana mara nne katika michuano hiyo.

Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola, ndio wanaaongoza kushinda mechi nyingi, ikiifunga mara tatu African Lyon huku yenyewe ikishinda mara moja tu (1-0), katika mchezo wa kwanza kabisa waliokutana Agosti 23, 2011.

Mechi tatu zote zilizofuatia hadi Lyon inashuka daraja msimu wa 2012/13, Azam FC iliibuka kidedea kwa kuifunga mabao 2-1 (Januari 25, 2012), 1-0 (Oktoba 6, 2012) na 3-1 (Aprili 11, 2013).

Katika mechi zote nne, Azam FC ndio iliyofunga mabao mengi zaidi ikitupia sita katika lango la wapinzani wao hao, huku Lyon yenyewe ikitingisha nyavu za matajiri hao mara tatu tu.

Azam FC kufukuzia rekodi

Mbali na kunuia kutwaa taji la pili la ligi msimu huu, Azam FC itaingia kwenye patashika hiyo ikiwa na rekodi nzuri ya kushika nafasi mbili za juu kwa misimu mitano mfululizo na msimu mmoja (2013/14) ikiibuka mabingwa kwa mara ya kwanza bila kufungwa mchezo wowote.

Hivyo msimu huu utakuwa wa sita mfululizo ikifanikiwa kushika nafasi hizo mbili na itakuwa ni mara pili kama ikitwaa ubingwa huo, ambapo kwa mujibu wa kikosi cha timu hiyo, safari hii kimeimarika sana hali ambayo inatoa mwanga wa kufanya vizuri zaidi katika michuano yote inayoshiriki.

Na moja ya malengo makubwa ya makocha wapya wa Azam FC ni kuifanya Azam FC kuwa timu bora Afrika Mashariki na Kati na Afrika kwa ujumla hadi kufikia mwakani kuanzia kucheza soka zuri uwanjani na kupata matokeo bora kwenye mechi inazocheza.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video