Kituo bora nchini cha Matangazo ya moja kwa moja 'Live' ya kandanda, Azam TV kimethibitisha kurusha mechi ye leo ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Wenyeji Young Africans na MO Bejaia ya Algeria.
Azam TV kupitia ukurasa wao rasmi wa facebook wametoa majibu ya maswali mengi ya watu wanaouliza kama watakuwa 'Live' leo uwanja wa Taifa ambapo wamewahakikishia kuwa mechi hii si ya kukosa kupitia kwenye kioo cha TV.
Mtanange huo utaruka kupitia Chaneli namba mbili ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar, ZBC2 , ambayo inapatikana ndani ya king'amuzi cha Azam TV.
Ujumbe wa Aza TV ulio-postiwa jana kwenye Ukurasa wao wa facebook
0 comments:
Post a Comment