Kikosi cha Azam FC bado kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mechi mbili zijazo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) zitakazofanyika mkoani Mbeya, Tanzania Prisons (Septemba 7) na Mbeya City (Septemba 10).
Azam FC kwa siku ya pili leo imeendelea kuwakosa nyota wake saba walioko timu za Taifa, kipa Aishi Manula, nabeki Shomari Kapombe, David Mwantika, viungo Himid Mao, mshambuliaji ambaye ni nahodha John Bocco, wote wakiwa Taifa Stars na kiungo Jean Mugiraneza akiwa Rwanda 'Amavubi'.
Katika kukiangalia kikosi chake kilichobakia, Kocha Mkuu Zeben Hernandez, leo asubuhi aliwapima wachezaji kwa mechi ya mazoezi dhidi ya timu ya vijana 'Azam Academy), mchezo ulioisha kwa wakubwa kuwachapa wadogo zao mabao 3-0, yaliyofungwa na Mudathir Yahya, Shaban Idd na Ramadhan Singano.
Picha kwa hisani ya Azam FC
0 comments:
Post a Comment