Asamoah Gyan
ameshindwa kufuzu vipimo vya afya na
hivyo hatajiunga na Reading FC kwa mkopo.
Nahodha huyo
wa Timu ya Taifa ya Ghana alikuwa mbioni kujiunga na Reading kwa mkataba wa
mkopo wa mwaka mmoja akitokea klabu ya
China ya
Shanghai
SIPG.
Taarifa
zinaeleza kwamba, nyota huyo mwenye miaka 30 hajafuzu vipimo vya afya na
hataweza kuwa fiti kuichezea timu hiyo kwa wiki nane atazokuwepo klabuni hapo.
Gyan aliwahi
kutamba nchini England akiichezea Sunderland aliyojiunga nayo akitokea Rennes
ya Ufaransa mwaka 2010 na alikipiga kwa misimu miwili ndani ya paka hao weusi kabla ya kutimkia Al Ain ya Abu Dhabi ambapo alifunga magoli 73 katika mechi 65,
ikiwemo magoli 44 ndani ya msimu mmoja.
Mwezi Julai
mwaka 2015, alijiunga na timu ya China ya Shanghai SIPG – kwa mkataba
uliomfanya alipwe mshahara wa paundi laki mbili na Elfu 27 kwa wiki na kuwa
miongoni mwa wachezaji wanavuta fedha nyingi Ulimwenguni.
0 comments:
Post a Comment