Arsene Wenger amesema kwamba Arsenal itabidi iangalie ingalie suluhisho mbadala la beki wa kati kutoka ndani ya klabu kuelekea mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool, licha ya kuhusishwa na beki wa Valencia Shkodran Mustafi
Katika mchezo huo, Arsenal itawakosa mabeki wake Per Mertesacker na Gabriel Paulista ambao wote ni majeruhi pamoja na Laurent Koscielny ambaye amechelewa kujiunga na timu kutokana na kuwa mapumzikoni baada ya fainali ya Michuano ya Euro mwaka huu.
Taarifa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya habari vinaeleza kwamba, Arsenal wameshatuma ofa ya paundi mil 20 kwaajili ya kumpata Mustafu, huku zingine zikidai kwamba wameambiwa waongeze ofa mpaka paundi mil 30
Kutokana na janga hilo, Wenger hana budi kuwatumia Calum Chambers, Rob Holding, Krystian Bielik na beki wa kushoto Nacho Monreal ambaye anaweza kumbadilisha kwa muda na kucheza kama beki wa kati kutokana na hao wengine kuwa na uzoefu mdogo.
"Tuna wachezaji wawili mjeruhi ambao hatukutarajia ambao ni Mertesacker na Gabriel, na Koscielny amechelewa kuja, hivyo ni vigumu kumpa nafasi katika mchezo huo kutokana na kukosa kwake utayari wa mchezo," Wenger amesema.
"Inafedhehesha sana, lakini hakuna namna ndiyo sehemu ya mchezo, wakati mwingine inabidi kutafuta suluhisho ya jambo ambalo usingefanya kama ungekuwa hauna majeruhi.
"Tuna upungufu katika suala hili, beki wa kati ni nafasi ambayo inahitaji uzoefu zaidit. Bila shaka tutafanya utaratibu wa kuongeza mtu, tunalifanyia kazi suala hilo, lakini mpaka kufikia Jumapili, itabidi niwe nimeshapata suluhisho kutoka ndani."
Amesema beki mpya mwenye miaka 20 Holding, ambaye amesajiliwa mwezi uliopita kutoka Bolton Wanderers amefanya vizuri sana tangu apewe nafasi ya kucheza na kusisitiza kwamba anaweza kumpa nafasi siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment