Shkodran Mustafi |
Arsenal wametuma maombi katika klabu ya Valencia wakitaka kumsajili Mlinzi ,Shkodran Mustafi .
Jonny Evans |
Pia wameomba kumsajili nyota wa West Brom, Jonny Evans, lakini bado hawajaweka mezani dau kwa wachezaji hao wawili.
Kitu kibaya kwa Arsenal ni kwamba; nao Chelsea wameshaliongeza katika orodha ya wachezaji wanaotaka kuwasajili jina la mlinzi huyo wa zamani wa Everton, Mustafi, wakitaka kuimarisha safu yao ya ulinzi wa kati.
Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, unaonesha kuwa kama timu inataka kumsajili inatakiwa kuuvunja kwa paundi milioni 41, lakini Valencia wanaweza kufanya mazungumzo kama dau la paundi milioni 25 litawekwa mezani.
Per Mertesacker |
Arsenal wanahitaji kuongeza beki mpya kutokana na nahodha wao, Per Mertesacker kusumbuliwa na majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.
Beki huyo wa Ujerumani alipata majeraha hayo katika mechi ya ufunguzi wa maandalizi ya msimu mpya ambayo Arsenal walicheza na RC Lens.
0 comments:
Post a Comment