Saturday, August 20, 2016

Mabingwa Watetezi wa EPL Leicester City wameshindwa kuibuka na ushindi kwenye mechi ya pili mfululizo dhidi ya Arsenal ambao pia walikuwa wakisaka ushindi wao wa kwanza msimu huu kwenye dimba la King Power.

Timu zote zilikuwa zikisaka ushindi kwa mara ya kwanza baada ya Leicester kupoteza dhidi ya Hull City huku Arsenal wakipoteza dhidi ya Liverpool.

Refarii Mark Clattenburg alizomewa na mashabiki wa Leicester baada ya kuwanyima penati katika vipindi vyote viwili vya mchezo, ya kwanza ni pale Laurent Koscielny alipomkwatua Danny Drinkwater kabla ya Hector Bellerin kuonekana kumuangusha Ahmed Musa dakika za mwisho za kipindi cha pili.

Straika wa Leicester Jamie Vardy alishindwa kutamba dhidi ya klabu ambayo ilikuwa ikimhitaji hapo awali na kukataa ofa yao. Alijitahidi kupambana lakini juhudi zake ama ziliishia mikononi mwa Petr Cech au mashuti yake kutoka nje. 

Kipa wa Arsenal Petr Cech aliokoa hatari kutoka kwa Riyad Mahrez katika dakika za lala salama huku Arsenal wakipoteza nafasi ya wazi kipindi cha kwanza baada ya shuti la Alex Oxlade-Chamberlain kuokolewa na kipa wa Leicester Kasper Schmeichel.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video