Sergio Aguero anaweza kufungiwa michezo mitatu baada ya kumpika kiwiko beki wa West Ham Winston Reid jana na kuwa na uwezekano wa kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester United.
Mshambulizi huyo alimfanyia tukio hilo Reid kuelekea mwishoni mwa mchezo huo ambao City walishinda 3-1, mabao yaliyofungwa na Raheem Sterling (2) na Ferndandinho. Reid alitolewa mara moja baada ya tukio hilo na kocha wake Slaven Bilic amsema alifanya hivyo kutokana na sababu za kiufundi.
Mwamuzi wa mchezo huo Andre Marriner alikuwa karibu kabisa wakati tukio lile likitokea. Aliamuru ipigwe free-kick na imeonekana kwamba hakujua kama Aguero alifanya kitendo kile. Lakini pamoja na yote hayo FA wanaweza kuangalia upya video na kuitolea maamuzi.
Endapo Aguero atakumbana na adhabu hiyo, basi anaweza kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester United utakaopigwa Old Trafford Septemba 10, mchezo mwingine ukiwa dhidi ya Bournemouth kabla ya kumalizia na Swansea kwenye Kombe la EFL.
0 comments:
Post a Comment