Straika wa Manchester City Sergio Aguero amekutwa na hatia na Chama cha Soka England FA kwa kosa la kumpiga kiwiko beki wa West Ham Winston Reid
Aguero anaweza kukumbana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ikiwemo miwili ya Premier League dhidi ya Manchester United utakaofanyika Septemba 10 na Bournemouth Septemba 17.
Nyota huyo wa Argentina (28), anaweza pia kukosa mchezo wa Kombe la Ligi (EFL Cup) raundi ya tatu dhidi ya Swansea City.
Aguero kwasasa yuko nje akiuguza majeraha yake ya nyama za miguu.
Mwamuzi Andre Marriner hakuona tukio lile lililotokea dakika ya 76 ya mchezo wakati City wakishinda 3-1 dhidi ya West Ham Jumapili, na hivyo FA wameamua kuchukua adhabu baada ya kurudia kuangalia tukio hilo kupitia video (retrospective action).
Bado ana muda wa kukata rufaa mpaka kesho Jumatano saa 2 kamili usiku.
0 comments:
Post a Comment