Wednesday, July 20, 2016

Wakati dirisha la usajili majira ya kiangazi barani Ulaya likitarajiwa kufungwa Agosti 31 mwaka huu, timu zinaendeleza mawindo na leo tunakuletea dili ghali kumi zilizokamilika mpaka sasa sasa.
Chelsea wamwanga paundi milioni 30 kuinasa saini ya kiungo wa Leicester City N'Golo Kante. Je, Mfaransa huyo ni miongoni mwa usajili wenye thamani zaidi majira haya ya kiangazi?
Hapa tunakuletea usajili kumi uliokamilika wenye  thamani kubwa zaidi mpaka sasa.
Kwanza ni Mbrazil HULK kutua Shanghai akitokea Zenit St Petersburg kwa paundi milioni 46.1 baada ya kutamba kwa misimu minne akisaka kandanda la kulipwa nchini Urusi.
Usajili huo wa Hulk uliofanyika mwezi Juni mwaka huu, ndio wenye thamani kubwa zaidi katika ligi ya China majira haya ya kiangazi , ingawa mambo yanaweza kubadilika.
Pili ni SADIO MANE kujiunga na  Liverpool akitokea Southampton kwa paundi milioni 36.
Southampton na Liverpool, miaka ya karibuni wamekuwa na mahusiano mazuri ya kuuziana wachezaji na sasa Mane amewafuata Anfield wachezaji wenzake wa zamani, Adam Lallana, Dejan Lovren na Nathaniel Clyne .
Nne ni  Granit Xhaka – Kusajiliwa na Arsenal kwa paundi milioni 34 akitokea Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.
Xhaka amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arsenal wakati huu kocha Arsene Wenger akijaribu kuimarisha kiungo chake na usajili huo umeingia kwenye orodha ya dili zenye  thamani kubwa  zilizokamilika.
Tano ni MICHY BATSHUAYI – kuhama Marseille na kujiunga na  Chelsea  kwa dau la paundi milioni 33.2
Timu nyingi za ligi kuu ya soka ya England zilivutiwa na mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, lakini bosi mpya wa Chelsea, Antonio Conte ameshinda vita dhidi ya timu kama West Ham na Tottenham.
Mlinzi huyo wa Ujerumani amekuwa mchezaji mwingine wa Borussia Dortmund kujiunga na wapinzani wao wakubwa baada ya wachezaji wenzake wa zamani Robert Lewandowksi na Mario Gotze kufanya hivyo.
Saba ni N’Golo Kante  kutua Chelsea akitokea Leicester City kwa ada ya paundi milioni 30.
Kante alisaidia Leiceter kutwaa ubingwa wa kihistoria wa EPL na ndipo Chelsea wameamua kutikisa benki yao kwa kulipa dau hilo wakimsaini kwa mkataba wa miaka mitano.
Nane,  Eric Bailly -  kusaini Manchester United kwa paundi milioni 30 akitokea Villarreal ya Hispania.
Bailly alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa mkataba wa miaka minne na kocha wa Mashetani wekundu, Jose Mourinho.
Bayern Munich wamemfanya Sanches kuwa miongoni mwa usajili wenye thamani zaidi kwa wachezaji vijana.
 Baada ya kufunga magoli 11 na kutoa pasi za mwisho 15 kwenye mechi 31 za Bundesliga akiichezea Dortmund msimu uliopita, Wakali wa Old Trafford  hawakuona shida kuweka mezani mzigo huo kumnasa Mkhitaryan.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video