Tuesday, July 12, 2016

Legend wa Arsenal Henry akiwa na kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa London Colney.
Thiery Henry ametangaza kuachana na Arsenal baada ya kutoafikiana na Arsene Wenger juu ya ama kuendelea kuwa kocha wa vijana au kubaki kuwa mchambuzi wa kituo cha runinga cha Sky Sports
Sky Sports inamlipa Henry kiasi cha paundi milioni 4 kwa mwaka.
Taarifa za ndani zinadai kwamba kitendo cha Henry kuikosoa Arsenal mara kwa mara hasa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Olivier Olivier Giroud ndiyo sababu kubwa ya Wenger kumuondoa.
Henry amewahi kusema kwamba Arsenal wasingeweza kubeba ndoo ya EPL endapo wangeendelea kumtegemea mshambuliaji chaguo pekee klabuni hapo Giroud.
Wenger, ambaye hutumiwa mara kwa mara na kituo cha TV cha TV beIN Sports kama mchambuzi aliifikisha Arsenal nafasi ya pili nyuma Leicester kwa alama kumi.
Watu wengi wameshangazwa na uamuzi huo wa Wenger hasa ukizingatia historia kubwa aliyonayo Henry katika klabu hiyo.
Imefikia hatua mpaka baadhi ya watu kusema kwamba inawezekana Wenger ana hofu ya kunyang'anywa tonge mdomoni kutokana na mkataba wake kusalia mwaka mmoja.Hata hivyo Henry aliahidiwa kupewa pesa katika kazi yake hiyo ya kukinoa kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 18 licha ya kwamba alitaka kufanya kazi hiyo bure kabisa.
Akiwa na Arsenal, Henry alifanikiwa kubeba ndoo mbili za EPL na tatu za FA kwa kipindi cha miaka nane alichodumu klabuni hapo. Alifunga magoli 228 kwenye michezo 376 na kujengewa sanamu nje ya uwanja.
Hivi karibuni mchezaji mwenza wa zamani Tony Adams alijiunga naye kama kocha msaidizi wa Henry katika kikosi hiko cha vijana.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video