Nusu fainali ya pili ya Euro 2016 inarindima tena leo ambapo miamba miwili ya soka barani Ulaya Ujerumani na Ufaransa inakutana katika mchezo utakaofanyika majira ya saa 4 usiku kunako dimba la Stade Vélodrome jijini Marseille.
Taarifa za kila timu
Ujerumani leo hawatakuwepo na beki wao Mats Hummels ambaye anatumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano na vile vile Sam Khedira na Mario Gomez ambao wanasumbuliwa na majeraha.
Bastian Schweinsteiger anasumbuliwa na maumivu ya goti licha ya jana kufanya mazoezi na kuna uwezekano mkubwa leo akapata nafasi, hiyo ni kwa mujibu wa kocha wake Low.
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps anaweza kufanya maamuzi binafsi ama ya kuendelea kumtumia Samuel Umtiti kwenye safu yake ya ulinzi ama kumrejesha Adil Rami, ambaye amemaliza adhabu yake ya kukosa mchezo mmoja.
Kiungo N'Golo Kante pia anarudi kwenye timu baada ya adhabu yake ya kukosa mchezo mmoja kukamilika.
Kikosi cha Ufaransa kinaonekana kuwa kamili zaidi kutokana na kutokuwepo kwa majeruhi yeyote mpaka sasa.
Uchambuzi juu ya mchezo wenyewe.
Mara ya mwisho Ujerumani kukutana na taifa kwenye kwenye michuano ya kimataifa, ilikuwa ni dhidi ya Brazail katika Kombe la Dunia mwaka 2014 ambapo walishinda mabao 7-1 na kuwatupa nje na kufikisha idadi ya michezo saba ambayo walifanikiwa kuwatoa wenyeji kwenye Michuano ya Euro na Kombe la Dunia kwenye hatua ya nusu fainali.
Moja kati ya matokeo hayo ya ushindi ilikuwa dhidi ya Ufaransa mwaka 1982 katika moja ya michezo ya kukumbukwa katika historia ya ya Kombe la Dunia.
Baada ya sare ya kushangaza ya mabao 3-3, Ujerumani waliibuka washindi kwa mara ya kwanza kwa njia ya mikwaju ya penati kwenye Kombe la Dunia. Mchezo huo utabaki kwenye kumbukumbu daima kutokana na rafu mbaya aliyocheza kipa wa Ujerumani Harald Schumacher dhidi ya Patrick Battiston na kusababisha mchezaji huyo wa Ufaransa kutotolea nje huku akiwa amefungwa mipira ya kuongeza hewa na Oxygen baada ya kupata 'cracks' tatu kwenye fuvu lake na meno yake mawili ya mbele kung'oka
Schumacher akazidi kuongeza machungu zaidi baada ya kuokoa penati mbili na kuwatupa nje Ufaransa.
Gazeti la L'Equipe la nchini Ufaransa limeelezea kiwango cha Ufaransa dhidi ya Iceland kama "Presque Parfait" (kiwango kisichotia shaka). Siku ile safu yao ya ushambuliaji ilikuwa moto wa kuotea mbali huku wakishindana wao kwa wao kuwania kiatu cha dhahabu.
Kiwango hicho kimemwachia hofu kubwa kocha wa Ujerumani Joachim Low: "Italy ilikuwa ni timu iliyocheza kwa mbinu kubwa. Ni timu kubwa lakini yenye kutabirika kulingana na wanavyocheza," amesema.
"Lakini Ufaransa ni tofauti. Huwa wanabadilika mara kwa mara, yaani hawatabiriki hata kidogo,"ameongeza.
Hata hivyo Ufaransa hawajawafunga Ujerumani kwenye michuano yoyote mikubwa tangu mwaka 1958 na hivyo mchezo huu kuwa mgumu sana.
Rekodi ya michezo waliyopambana.
- Huu unakuwa ni mchezo wa tano katika ya Ujerumani na Ufaransa katika michuano mikubwa, lakini mara ya kwanza kwenye Michuano ya Ulaya.
- Ufaransa kwa mara ya kwanza kabisa walishinda dhidi ya Kombe la Dunia mwaka 1958 wakati Ujerumani wakafanya hivyo kwenye michuano mitatu iliyofuata (1982, 1986 na 2014).
- Ujerumani na Ufaransa wameshinda asilimia 36 ya fainali zote za Michuano ya Ulaya (tano kati ya 14). Wao ndio wanaongoza kwa kufunga magoli mengi zaidi katika historia ya michuano hiyo (magoli 72 kwa Ujerumani na 6o kwa Ufaransa).
- Alain Giressa ndiye mchezaji wa mwisho wa Ufaransa kufunga dhidi ya Ujerumani katika michunao mikubwa, ilikuwa ni kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1982.
- Mara ya mwisho walikutana Novemba 2015, Ufaransa walishinda 2-0 kwenye mchezo ambao kulizuka mashambulizi ya kigaidi jijini Paris.
- Ufaransa hawajapata clean sheet kwenye michezo yao minne iliyopita dhidi ya Ujerumani kwenye michuano mikubwa.
Germany
- Ujerumani wamefanikiwa kufika nusu fainali kwenye michuano michuano yote sita iliyopita, wakiwa wanaoongoza kuliko timu yoyote Ulaya.
- Miaka 20 bila ya kuchukua kombe la Ulaya ni kipindi kirefu zaidi kwenye historia ya michuano hii.
- Wamepoteza mchezo kati ya 18 iliyopita kwenye michuano mikubwa (kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Italy kwenye Euro ya mwaka 2012).
- Thomas Muller hajafunga hata goli moja kwenye michezo 10 ya Euro mwaka huu. Vile vile alikosa mkwaju wa penati kwenye mchezo dhidi ya Italy Jumapili iliyopita. Ana magoli 10 kwenye michezo 13 ya Kombe la Dunia.
Ufaransa
- Ufaransa wameingia nusu fainali katika michuano mikubwa kwa mara ya kwanza tangu Kombe ka Dunia mwaka 2006. Wamefanikiwa kufuzu kwenda fainali mara 3 kati ya mara tano zilizopita walizofika nusu fainali, huku mara ya mwisho kushindwa ilikuwa mwaka 1996 dhidi ya Jamhuri ya Czech.
- Hawajafungwa kwenye michezo yao 17 iliyopita katika mashindano mbalimbali yaliyofanyika ardhi yao ya nyumbani, wameshinda 15 na kutoaka sare mara mbili. Mara ya mwisho kufungwa ilikuwa ni kwenye uzinduzi wa Michuano ya Ulaya mwaka 1960.
- Ufaransa ndio wanaongoza kwa magoli kwenye michuano ya mwaka huu wakiwa na magoli 11 kwenye michezo 5. Mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni kwenye Euro ya mwaka 2000 (13)
- Wamefunga magoli matano ya kichwa, rekodi nyingine hiyo kuwekwa na timu moja kwenye msimu mmoja wa michuano ya Euro.
- Olivier Giroud amefunga kwenye kila mchezo kati ya michezo miwili aliyoanza. Goli lake la kwanza kwa Ufaransa alifunga February mwaka 2012 jijini Bremen dhidi ya Ujerumani. Amemfunga Manuel Neuer mara tatu alizokutana naye (mara moja akiwa Ujerumani, mara mbili Arsenal vs Bayern)
- Giroud amefunga magoli manne na kutoa pasi tatu za magoli kwenye mechi sita alizoanza kwenye michuano ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment