kiungo mahiri wa mabingwa wa kandanda wa ligi kuu ya England, Leicester City na timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, N’Golo Kante amesajiliwa na Chelsea.
Nyota huyo aliyeisaidia Leicester City kubeba ubingwa chini ya kocha wao, Claudio Ranieri, amejiunga na Chelsea kwa dau la pauni million 30 na mwenye amethibitisha akisema kujiunga na klabu hiyo ni sehemu ya kutimiza ndoto zake.
Chelsea kupitia akaunti yao ya Twita walimkaribisha Kante kwa maneno yanayotafsuriwa: "Ni Rasmi, karibu Chelsea, N'Golo Kante!"
0 comments:
Post a Comment