Cristiano Ronaldo anaweza kuwa amecheza dakika 25 tu za mchezo wa fainali ya Euro dhidi ya Ufaransa, lakini staa huyo wa Real Madrid bado ndiyo mtu anayeongelewa zaidi kuliko mtu yoyote yule.
Mreno huyo ambaye ametaa Ballon D’Or mara tatu aliumia katika dakika za awali za mchezo baada ya kufanyiwa madhambi na kiungo mshambuliaji wa Ufaransa Dimitri Payet.
Licha ya kujitahidi kuvumilia ili aendelee kucheza, lakini ilishindikana.
Baadaye akiwa nje Ronaldo alijikuta akiwa kocha msaidizi baada ya muda mwingi kuutumia akitoa maelekezo kwa kusaidiana na kocha wake Fernando Santos.
Baada ya jeraha hilo mama yake Cristiano Ronaldo Dolores Aveiro aliamua kundika kwenye Twitter kuonesha namna gani alivyoumizwa na kitendo alichofanyiwa mwanaye.
‘Nimeumizwa sana kumuona mwanangu aiwa kwenye hali hii. Mchezo wa soka uhahusisha kuchezea mpira, na sio kumuumiza mpinzani soka.’
0 comments:
Post a Comment