Thaban Scara Kamusoko ni moja ya wachezaji hodari wa kigeni anayekipiga kunako Ligi Kuu Tanzania Bara.
Nyota huyu Mzimbwe katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu ya Yanga amefanikiwa kutoa mchango mkubwa sana katika kufanikisha ubingwa wa klabu hiyo
Mwishoni mwa wiki hii wakati wa ugawaji tuzo mbalimbali kwa timu na wachezaji waliofanya vyema, Kamusoko alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi wa kigeni.
Alionekana kuwa na furaha lakini mwenye hekima kubwa. Kamusoko alishinda tuzo hiyo baada ya kumsinda Mzimbabwe mwenzake Donald Ngoma.
Baada ya tuzo hiyo, Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kamusoko aliandika maneno haya: "Wana take this opportunity to thank all those who have stood by me the last season....it was really a good season for me and my team Yanga...and to thank Vodacom sponsors for choosing me as the best foreign player not forgeting the supporters of @Young Africans.....now focusing on the next coming season...stay blessed."
Akimaanisha kwamba...ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote waliochangia mafanikio yangu msimu uliopita....ulikuwa ni msimu mzuri mno kwangu na timu yangu ya Yanga...na vile vile nawashukuru sana Vodacom ambao ndio wadhamini wa ligi hii kwa kunichangua kuwa mchezaji bora wa kigeni bila kusahau mashabiki wa Yanga....sasa kilichobaki ni kusubiri mapambano kwa ajili ya msimu ujao....nyote m'barikiwe.
0 comments:
Post a Comment