Jana Pep Guardiola amenza rasmi kuonja ladha ya kusimama katika benchi la Manchester City kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Bayern Munich. Namna alivyokuwa akitoa viashrio vyake unaona kabisa kuna habari mpya. Alikuwa akirusha mikono mara nyingi tofauti na alivyozoeleka mara nyingi kuweka mikono mfukoni. Uso wake mara nyingi ulikuwa hauja-relax kama ambavyo imezoeleka. Muda wote alionekana si mwenye utulivu bali kutoa maelekeza kwa wachezaji wake.
Ni wazi kwamba, lazima haya yangetokea kwenye mchezo wa kwanza kabisa Guardiola akiwa kocha wa Manchester City. Hata kama ulikuwa ni mchezo wa kirafiki dhidi ya waajiri wake wa zamani, lakini Guardiola ni kocha ambaye anapenda kusimamia sana falsafa yake ambayo ni kucheza soka la pasi nyingi. Ikumbukwe kwamba alikuwa akichezesha vijana ambao hawako 'familiar' na mfumo wake na kubwa zaidi bado hajakaa nao kwa muda mrefu.
Kama uliangalia vizuri mchezo wa jana,basi uliona tofauti kubwa sana kati ya Guardiola na Ancelotti. Mara nyingi Ancelotti alionekana kutulia hakuwa na mchecheto. Lakini Guardiola alionekana ni mwenye mizuka mingi na mara kadhaa alivuka mstari wa eneo lake la kujidai na kusababisha mwamauzi wa akiba kumrudisha. Unajua kwanini? Bado vijana wake hawajaupata vizuri mfumo wake.
Licha ya kwamba hiyo ni haiba ya Guardiola, lakini kikubwa zaidi ni kwamba anahitaji kupandikiza mfumo wake kwenye timu yake hiyo tofauti na Ancelotti ambaye alikuwa anatafuta namna mpya tu ya kutengeneza nafasi na sio kutengeneza mfumo.
Baada ya mchezo wa kumalizika na kuelekea kwenye chumba cha mkutanO na wanahabari, Ancelotti aliulizwa maswali juu ya mchezo huo na kusema kwamba mechi ile inaweza kujirudia kwenye fainali ya Uefa mwakani, lakini kwa upande wake Guardiola akakataa kabisa. Unajua kwanini? Kwa sababu ana kibarua kikubwa cha kufanya.
Alisema: "Kwa upande wa Manchester City, mwaka jana ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Hawajawahi kufika fainali hata mara moja, hivyo basi historia yetu kama klabu haifanani kabisa na historia tuliyonayo kwenye Michuano ya Uefa.
"Lazima niwe muwazi. Mimi sidhani kama tunaweza kufika huko kote. Hakuna shaka kwamba tutajaribu kucheza kwa kadri tuwezavyo, kila baada ya mchezo mmoja tujitahidi kuimarika. Tutajaribu kufanya hivyo. Lakini kwa sasa, hatupo hata kwenye Ligi ya Mabingwa. Kilichopo hapa ni kujaribu kwanza kufuzu halafu mengine yatafuata."
Mchezo wa jana ulikuwa mgumu kidogo kwake kutokana na kuwakosa wachezaji muhimu katika kikosi chake kama Sergio Aguero na Kevin De Bruyne ambao bado wako mapumziko baada ya kumaliza kuzitumikia timu zao za taifa kwenye Michuano ya Copa America Centenario na Euro 2016 mtawalia. Vincent Kompany na kiungo mpya Ilkay Gundogan bado wako nje wakiuguza majeraha yao.
Ukosefu wa nyota hao ulitumiwa kwa usahihi na Bayern ambao walikuwa na nyota wake kama Franck Ribéry, Javi Martínez, Xabi Alonso, Philipp Lahm na David Alaba wote wakiwa kwenye kikosi kilichoanza jana. Kabla ya kutolewa wakati wa mapumziko, Ribery hasa-hasa alionekana kuinyanyasa sana safu ya ulinzi ya City ambayo ilikuwa chini ya Aleksandar Kolarov ambaye asili yake ni beki wa kushoto.
Baadaye Kolarov alitolewa na kuingia Gael Clichy ambaye pia si nafasi ya beki wa kati si asili yake. Na Guardiola alipoulizwa kama utakuwa ndiyo mfumo wake alikata na kusema kwamba hiyo ni muda mfupi tu.
"Kolarov yuko imara kwa mipira ya juu, ni mchezaji mwenye kasi, ana uwezo mkubwa wa kutengeneza mashambulizi kutokea nyuma. Lakini ni beki wa pembeni," alisema. Kwa sasa kwenye timu hatua beki yeyote wa kati..wote ama wako kwenye mapumziko au wanauguza majeraha. Na ndio maana tumemchezesha Clichy kama beki wakati pia. Hatukuwa na suluhisho juu ya hili kwa leo."
Pengine wengine watakuja zaidi siku zijazo. City bado wanahusishwa na usajili wa beki kisiki wa Juventus Leornado Bonucci, licha kwamba Mabingwa hao wa Italia wanaonekana kuweka kizingiti cha kumzuia beki huyo kuondoka. Pia kuna tetesi za kumchukua John Stones kutoka Everton. mchezo wa jana ulikuwa mahususi kabisa kwa Guardiola kukikfanyia tathmini kikosi chake kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi.
Kulikuwa na viashirio vizuri kutoka kwa kinda kutoka Ukraine Oleksandr Zinchenko ambaye alionesha kuwa mwepesi na mjanja kutokea pambeni mwa uwanja, bila kusahau Angelino kutoka Uhispania ambaye allicheza vizuri sana katika nafasi ya beki wa kushoto kabla ya kuhamishiwa kucheza kama winga baadaye. Wachezaji wote hao ndio kwanza wana miaka 19.
Licha ya kutopata nafasi kubwa msimu uliopita, kipa Caballero anaweza kufikiriwa upya na Gurdiola kutoka na kiwango chake alichokionesha jana bila kusahau kipa mwingine kinda aliyeingia kuchukua nafasi yake Angus Gunn ambaye kwa bahati mbaya aliruhu gaoli pekee katika mchezo wa jana.
Mbali na hayo yote Guardiola hatasahau mambo mzuri aliyokuta kwa Bayern ambao ndio waajiri wake wa zamani baada ya kumkaribisha kwa bashasha huku wakiweka bango kwenye eneo la kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo lililokuwa limeandikwa "Welcome Back." ambapo pia kulikuwa na picha yake.
Mashabiki wa Manchester City watakuwa na furaha baada ya kuanza kuona mabadiliko kidogo kwenye timu yao ambayo wanhisi utakuwa na mwanzo mzuri wa mafanikio ya timu yao licha ya kupoteza mchezo wa jana. Chemistry ta timu ilionekana, wachezaji walikuwa hawauogopi mpira.
Hawapaswi kufukiri mafanikio ya moja kwa moja kwa haraka, lakini wanapaswa kusubiri Gaurdiola apandikize mbegu zake kwenye timu kisha kuanza kula mataunda ya mafanikio baada ya muda. Guardiola ni kocha mzuri, hilo halina shaka na akipewa muda City wanafurahia maisha kwenye mchezo wa soka.
0 comments:
Post a Comment