Werner Mickler, mwanasaikolojia wa michezo ambaye anafanya kazi bega kwa bega na chama cha soka nchini Ujerumani anasisitiza kwamba wachezaji wanatakiwa kuwa na fikra chanya tu kuelekea mchezo robo fainali ya Euro mwaka 2016 dhidi ya Italy utakaofanyika kesho.
Mwanasaikolojia huyo wa kiwango cha juu kabsa anasisitiza kwamba, kocha na wachezaji wa hawapaswi kuangalia rekodi mbovu ya Ujerumani dhidi ya Italy kuelekea mchezo huo wa kesho.
Timu hizi mbili zimekutana mara nane katika michuano mbalimbali mikubwa ulimwenguni, na katika michezo yote hiyo Ujerumani hajawahi kupata ushindi hata mara moja kwa takriban zaidi ya miaka hamsini.
Mabingwa hao watetezi wa Kombe la Dunia mara ya mwisho kukutana na Italy ilikuwa ni kwenye mechi ya kirafiki mwaka uliofanyika mwezi March na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 yaliyofungwa na Toni Kroos, Mario Gotze, Jonas Hector na Mesut Ozil.
“Timu unayoihofia inaweza kudumu kwenye fikra zako kwa muda mrefu,” mwanasaikolojia wa michezo Werner Mickler ambaye anafanya kazi na makocha kupitia chama cha soka nchini Ujerumani ameuambia mtandano wa Goal.
“Sasa hapa kuna suala la namna ambavyo wachezaji wanalichukulia jambo hili. baada ya hapa tunaangalia namna gani ya kukabiliana nalo."
“Unatakiwa kufahamu kwamba Ujerumani walibeba Kombe la Dunia na walimudu changamotto zote kuelekea mafanikio yao, maana yake unapata nguvu kubwa ya kujiamini. Zaidi ya hapo, mara nyingi watu hufikiri kilichotokea wakati uliopita basi kitatokea tena wakati ujao. Lakini sivyo, kila mechi inakuwa na changamoto mpya. Hivyo inategemea na namna ambavyo unakabiliana nayo kama mchezaji au timu.
“Rekodi mbaya katika michuano ndiyo inaweza kuwa changamoto ya kukupa nguvu ya kupambana pia. Unakuwa unataka kuonesha namna gani unaweza kukabiliana nayo.
“Ubingwa wa Kombe la Dunia na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa kirafiki Italy unaonesha kwamba mnaweza kufanya kitu cha tofauti, na hilo ndilo suala la msingi.
“Unakuwa na uwezekano mkubwa wa kumfunga aina hii ya mpinzani. Tunahitaji kuwa na siku mujarab kuweza kukabiliana na hali hii kwa mafanikio, na kumbuka kwamba tunahitaji kukumbuka mambo yote ambayo yana mtazamo chanya kwetu. Unaweza kufananisha mechi hii na mwanafunzi anayekabiliana na mtihani huku akiwa na hofu. Kama mtu huyu anafirikia mtihani tu....basi hawezi kufeli kwasababu atakuwa anafikiria namna gani ya kukabiliana nao."
Kwa mara ya mwisho kwenye mechi za kuishandani, Ujerumani ilikutana na Italy kwenye Euro ya mwaka 2012 na kukubali kipigo cha mabao 2-1 yaliyofungwa na Mario Balotelli wakati huo.
Lakini Mickler amesisitiza kwamba kuangalia matokeo ya mechi zilizopita si jambo linalopaswa kuwekwa akilini mwa wacheza na anataraji kumwona Low akiweka mipango thabiti kuwadhibiti vilivyo Italy hapo kesho.
“Ni muhimu zaidi kuangalia suluhisho. Hautakiwi kufukiria sana juu ya ubora wa mpinzani wako, unahitaji kuwakubali. Lakini siku zote udhaifu haukosekani vile vile na unachotakiwa ni kuutumia kikamilifu kujinufaisha,” amesema.
“Unatakiwa kuwa na ushawishi kwamba mkakati wako unaweza kufanya kazi na awali ya yote unakuwa na suluhisho tofauti tofauti. Hivyo basi hata kama mpango A haujafanikiwa, unatumia mpango B na baadaye mpango C, na hapo sasa utajisikia mtu ambaye yuko salama kabisa."
“Wakiwa kama Mabingwa wa Dunia, Ujerumani wanafahamu jinsi gani ya kuusoma mchezo, ni muhimu kuwa wa kwanza kumfanya mpinzani akuogope na sio wewe kumuogopa"
“Kama Ukiruhusu goli bado unatakiwa kufahamu kwamba unaweza kuondokana na hali hiyo. Hivyo basi unahitaji mpango B. Kama unakuwa wa kwanza kuruhus goli, kunakuwa na taswira inayojengeka kwenye akili yako, hilo ni suala tofauti kwa mmoja mmoja. Na kama hiyo ndio sababu, unakiwa kuzuia taswira hizo na kuanza kukumbuka nini hasa ulijifunza katika kipigo cha mwaka 2012.”
0 comments:
Post a Comment