Taarifa:
Mpaka sasa klabu ya Ndanda FC imemsajili mchezaji mmoja tu kutoka Geita Gold SC, Ibrahim Hassan Isihaka ' Mamba'.
Huyu ni mchezaji wa zamani wa Tanzania Prisons. Pia alicheza mwanzoni mwa Msimu uliopita Ndanda FC kabla ya kuondoka dirisha dogo klabuni hapo kujiunga na Geita Gold iliyokuwa chini ya Seleman Matola.
"Tumemsajili mchezaji mmoja tu, Ibrahim Hassan Isihaka maarufu Mamba na kuwaongezea wachezaji wetu wengi mikataba". Idrissa Bandali, Msemaji wa Ndanda ameiambia MPENJA SPORTS!! na kuongeza: "Hassan Isihaka hatujamsajili na wala hatujaanza kuzungumza naye. Hizo ni Habari tu, hazina ukweli".
0 comments:
Post a Comment